YANGA IPO TAYARI KUIVAA BLACK LEOPARD KESHO



Kikosi cha Young Africans Sports Club
Timu ya Young Africans ambayo ilikuwa imeweka kambi ya mafunzo takribani wiki mbili mjini Antlaya nchini Uturuki kesho siku ya jumamosi itashuka dimba la Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini.
 
Black Leopard timu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini maarufu kama PSL inatazamiwa kuwasili mchana huu kwa shirika la ndege la South African Airways ikiwa na msafara wa watu 42, ambapo timu pamoja na viongozi wake watafikia katika hotel ya White Sands Mbezi Beach.
 
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga tangu kurejea nchini, hivyo ni nafasi kwa wadau, wapenzi wa soka kufika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuweza kujioniea mchezo huo majira ya saa 10 jioni siku ya jumamosi.

Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kutoka katika ligi kuu ya PSL nchini Afrika Kusini hivyo atatumia nafasi hvyo kukamilisha maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.

Leo asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Mabatiini Kijitonyama tayari kabisa kujianda na mchezo huo.
 
Wachezaji wote wameendela na  mazoezi leo isipokuwa Hamis Kiiza 'Diego' na mlinda mlango Yusuph Abdul ambao wanaoumwa malaria.
 
Aidha katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amemtambulisha Dr Nassoro Matuzya kwa wachezaji leo asubuhi kama dakatari wa timu ambapo ameanza kazi kushika nafasi ya daktari aliyekuwepo Dr Suphian Juma.

Comments