WASHIRIKI WA FAINALI ZA TAIFA ZA MISS UTALII HADHARANI


Fainali za mashindano ya Miss Utalii Tanzania na mchakato wa kuwapata wawakilishi wa mikoa katika Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania umekamilika katika mikoa yote ya Tanzania.
Mikoa hiyo na majina ya warembo katika mabano ni Arusha(Rose Godwin),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas), Dar es Salaam 1(Sophia Yusuph 21) ,Dar es Salaam 2(Ivon Stephen,21) ,Dodoma(Erica Elibariki,20), Geita (Jamia Abdul,19), Iringa(Debora Jacob Mwansepeta ), Kagera (), Kilimanjaro(Anna Pogaly,23), Kigoma ( Zena Sultan,18), Katavi (Asha Ramadhani,22), Lindi (Joan John,18), Mara(Doreen Bukoli,18), Mbeya (Dayana Joachim,19), Mwanza(Jessica Peter Rugalabamu,18), Mtwara (Halima Hamis Suleman,19), Morogoro ( Hadija Saidi,21), Manyara (Mary Chrysostom Rutta,18) Njombe (Paulina Renard Mgeni,20), Pwani (), Rukwa (Anganile Rogers Emmanuel ,22), Ruvuma( Furaha Amon Kinyunyu ,23), Singida (Neema Julius,20),  Simiyu (Flora Msangi,22), Shinyanga (Lightness Kitua,19),Tabora (Magreth Michael Malale,20 ),Tanga (Sarafina Jackson Chales,18),Vyuo Vukuu 1(Irine Richard Makoye,21), Vyuo Vikuu 2 (Hawa Nyange, 22)
Washindi wa kwanza na wa pili wa kila mkoa watawakilisha mikoa yao, katika Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,fainali ambazo zimepangwa kufanyika mwushoni mwa mwezi huu,katika Ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam. Fainali za mwaka huu zitatanguliwa na kambi ya siku 21 ya washiriki wote itakayo kuwa katika Hoteli ya kitalii ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam.
Maandalizi kwaajili ya kuanza rasmi kambi ya Taifa yanaendelea na yamekamilika kwa zaidi ya 96%,tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha Taratibu za Baraza La Sanaa la Taifa,ukiwemo kulipa ada ya shindano ya shilingi 1,500,00.00,kabla ya uzinduzi rasmi wa kambi utakao fanyika katika hoteli ya Ikondelelo, Kibamba Dar es Salaam,tarehe 8-1-2013.
Washiriki wote watawania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/13 .sambamba na tuzo 28 mbalimbali za heshima za Jamii, Elimu ya Jamii, Afya ya Jamii,Utalii, Utamaduni, Uchumi, Miundo Mbinu ya Utalii, Uwekezaji ,Madini na Maliasili mbalimbali za Taifa.
Fainali za Taifa za mwaka huu ,zitakuwa ni za Tano tangu kusajiliwa rasmi na serikali na mamlaka za haki miliki za kutaifa na kimataifa mwaka 2002,katika kipindi hicho tumefanikiwa kutwaa mataji katika kila mashindano ya Dunia na kimataifa tuliyoshiriki,ambapo hadi sasa tunashikilia zaidi ya mataji matano ya Dunia na kumataifa. Mataji hayo ni pamoja na Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism world 2006-SADC, Miss Tourism World 2007-Africa,Model Of The World 2006-Personality, Miss Africa 2006-1ST Runner Up na Miss Tourism World 2008-Internet.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais/Afisa Mtendaji Mkuu

Comments