WASANII KIBAO KUPAMBA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA


Umati wa watu kutoka kila pande ya dunia unatarajiwa kukusanyika  pamoja mwezi wa pili Mjini Zanzibar kusherekea miaka 10 ya tamasha la muziki la Sauti za Busara. Tamasha hili litaanza tarehe 14 mpaka 17 Februari 2013 ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar. Tamasha litavutia idadi kubwa ya wenyeji na wageni kutoka mataifa mbali mbali kwa mwaka2013.  Tamasha litasherekea mafanikio yake ya kuwajumuisha wasanii na watazamaji pamoja kutoka kila pande ya Afrika na kwengineko kwa utajiri wetu wa utamaduni na uzoefu,  kukuza utamaduni na maendeleo katika jamaii kwa miaka 10 iliyopita.
Sauti za Busara ni tukio la kipekee la kila mwaka Afrika mashariki na linajulikana kama ‘ Tamasha rafiki  zaidi duniani’.  Katika toleo hili litajumuisha wasanii 200:  zaidi ya vikundi ishirini na tano kutoka Afrika mashariki na kwingineko;  utaalamu wa kutumia vyombo vya umeme na asilia  vyote hivi vitaonekana moja kwa moja kwenye jukwaa la Sauti za Busara.
Ndani ya Ngome Kongwe itakuwa ni siku tatu mfululizo kwa muziki wa moja kwa moja, ratiba  hii itaendelea  kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili ikiambatana na shoo kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa saba usiku
.
Tamasha pia litajumuisha filamu za miziki ya kiafrika: kumbukumbu, video za muziki na maonyesho ya moja kwa moja ya onyesho, yote haya tumelenga kukuza utajiri na utofauti wa muziki wa kiafrika hii itaonyeshwa ndani ya ukumbi wa Amphitheatre Ngome Kongwe

Kiingilio katika tamasha kwa Watanzania ni 3,000/- TSh.
Orodha ya wasanii wa kimataifa watakao shiriki Tamasha la 10 la Sauti za Busara ni Cheikh Lo kutoka Senegal,  ni mwimbaji, mwandishi, mpiga Gitaa, Kora, ngoma na ni kivutio Afrika magharibi na kati, aliunda aina yake ya  kipekee. Cheikh Lô alizaliwa mwaka 1955, wazazi wake ni watu wa Senegal mji wa Bobo Dioulasso, Burkina Faso, sio mbali na mpaka wa Mali,mahali alipokulia wanaongea Bambara (Lugha ya  Mali), Wolof (Lugha ya Senegal) na kifaransa.  Wakati wa utotoni alikuwa anasikiliza aina zote za muziki hususani miziki ya Congo ijulikanayo kama rumba ni muziki unaojulikana sana Afrika. Miaka 21 alianza kuimba na kupiga kora na Orchestra Volta Jazz mjini  Bobo Dioulasso. Youssou N'Dour  aliitambua sauti yake ndipo alipomsaidia kukuza kipaji chake baada kukutananaye  kwa mara ya kwanza  mwaka 1989. "Kila alipokuwa akiimba vibwagizo nilivutiwa na sauti yake," N'Dour alisema, " lakini nilitokea kumfahamu kupitia nakala yake 'Doxandeme'.  Niliisikiliza sauti yake "wow" – Niliona kitu kupitia sauti yake ambayo ilikuwa safari kutoka Burkina, Niger, Mali".
Katika Tamasha la miaka 10 ya Sauti za Busara itakutanisha bendi bora (Best of the Best) ambazo zilipendwa na mashabiki wa muziki kwa miaka tisa iliyopita ikiwemo bendi Mama na kiongozi wa rumba Tanzania wanaojulikana kama DDC Mlimani Park Orchestre (Sikinde)
Nao wakati wa Taarab asilia Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla wajulikanao kama Culture Musical Club wataonyesha cheche zao kwenye Tamasha la kumi la Sauti za Busara, kundi hili lililojizolea umaarufu sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kama Marekani, Japan na kwingineko.
Wasanii wengine ni Khaira Arby (Mali), Comrade Fatso na Chabvondoka (Zimbabwe),  Atongo Zimba (Ghana),  N'Faly Kouyaté (Guinea),  Nathalie Natiembe (Reunion),  Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte), Wazimbo (Mozambique), The Moreira Project (Mozambique / Afrika Kusini), Owiny Sigoma Band (Kenya / UK), Mokoomba (Zimbabwe), Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania), Mani Martin (Rwanda), Burkina Electric (Burkina Faso / USA),  Lumumba Theatre Group (Tanzania), Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden), Super Maya Baikoko (Tanzania), Peter Msechu (Tanzania)   na wengineo wengi.
Sauti za Busara itaandaa Movers & Shakers networking forum kwa wenyeji na wageni wataalam  katika sanaa. Mtandao huu utachukuwa nafasi  katika kujadil maendeleo,  kubadilishana mawazo  na ubunifu katika kiwanda cha sanaa kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko.
It’s not just the festival that puts on a show; the local community is encouraged to take part by hosting Busara Xtra fringe events. These includetraditional ngoma drum and dance, fashion shows, dhow races, open-mic sessions, after-parties and performances of Zanzibar’s oldest taarab orchestras as arranged by the local community. 
Si tamasha pekee linalofanya maonyesho: wenyeji nao wanapewa moyo wa kuhodhi matukio mbalimbali yajulikanayo kama Busara Xtra. Matukio hayo yanajumuisha ngoma za asili, maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa, taarabu asilia na mengineyo mengi ambayo yanaandaliwa na wenyeji.