WANACHAMA SIMBA NA YANGA WAHIMIZWA KULIPIA ADA ZAO KUTUMIA M-PESA


Taarifa kwa vyombo vya habari
Wanachama Yanga, Simba waaswa kulipia ada  kupitia M-pesa.
Dar es Salaam (3 January 2013) –Kutokana na kukua kwa kasi kwa maendeleo ya teknolojia katika sekta ya soka nchini –klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zimeaswa kuwahamasisha wanachama wa klabu hizo kulipia ada ya uanachama kupitia huduma ya M -Pesa.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kuwa hali hiyo itasaidia kuepusha ubebaji wa fedha taslimu mbali na hivyo, pia zoezi hilo liitapunguza upotevu wa muda wa wanachama kutoka sehemu moja hadi nyingine na kwenda klabuni kulipia ada ya uanachama.
“Iwapo vilabu vya soka nchini vitawaahamasisha wanachama wake kutumia huduma ya M-Pesa  kulipia ada ya uanachama wataweza kuoka muda wa kwenda klabuni, wataokoa gharama na pia kutakuwa na usalama wa fedha zao,” Bw. Twissa alisema.
Aidha, Bw. Twissa aliongeza kuwa kutokana na utumiaji wa malipo kwa huduma ya M-Pesa –mapato ya vilabu pia yatakuwa salama.
Hivi karibuni mhasibu wa klabu ya soka ya Simba, alivamiwa na kuporwa fedha za mapato ya klabu hiyo zilizotokana na mgawo wao wa mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na klabu ya Tusker ya Kenya.
Bw. Twissa, anaamini kuwa kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo ya ulipaji wa ada ya uanachama kwa vilabu kwa kupitia huduma ya M-Pesa itasadia kuchochea ongezeko la idadi ya wanachama kwenye vilabu hivyo pamoja na uhai wa wanachama hao.
“Huduma hii ya M-Pesa nina imani itakapoanza itasaidia kuongeza idadi ya wanachama wapya kwenye vilabu na hata kuongeza mapato ya vilabu. Kuna wanachama wengine ambao wanashughuli nyingi ambapo kwao kupata ule muda wa kufanya mambo kama hayo ni nadra sana lakini pia kuna wengine wao wanapata uvivu wa kwenda kulipia ada hiyo,” alisema.
Huduma ya M-Pesa nchini imekuwa ikikuawa kwa kasi ambapo imeweza kurahisisha maisha ya wananchi kwa ujumla kwa kupata mahitaji ya kila siku ya binadamu. Hivi karibuni, Vodacom Tanzania imeingia mikataba na Shoppers Supermarket kwenye maeneo ya Msasani na Masaki.

Comments