WAGOMBEA URAIS TFF WAFIKA WATATU, 30 JUMLA WACHUKUA FOMU

Manji akizungumza na Waandishi leo baada ya kuchukua fomu

Na Boniface Wambura
WADAU watatu wa soka nchini, leo mchana wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitokeza hadi sasa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.
Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

MANJI NAYE ACHUKUA FOMU TFF, KUMEKUCHA


Manji anazungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu

Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ akimchukulia fomu ya kugombea Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa niaba ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Mehbub Manji (kulia) ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayetoa fomu hiyo kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   

Zamunda anamkabidhi fomu yake Manji
Mhasibu wa TFF anamuandikia Manji risiti

MALINZI AREJESHA FOMU YA KUOMBA URAIS TFF, ALICHUKUA KWENYE MTANDAO

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi akirejesha fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ofisi za shirikisho hilo, Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayepokea fomu hiyo ambayo Malinzi alichukua kwenye tovuti ya TFF na kujaza kisha kuilipia katika benki ya CRDB kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   
Anashuka kwenye gari

Anaanza kuekelea ofisi za TFF
Anajiorodhesha
Risiti yake ya benki
  
Anazungumza na Waandishi wa Habari

MTOTO WA TMK NYAMLANI WA KWANZA KUCHUKUA FOMU URAIS TFF


Makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Jumanne Nyamlani akichukua fomu ya kugombea urais wa shirikisho hilo, kwenye ofisi za TFF, Ilala, Dar es Salaam mida hii kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayekabidhi fomu kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.

Akiwa na rafiki zake waliomsindikiza kuchukua fomu
Anahesabu fedha

Makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Jumanne Nyamlani akikabidhi fedha za malipo ya fomu ya kugombea urais wa shirikisho hilo, katika uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayepokea kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya