VITALIS MAEMBE 'SUMU YA TEJA' KUANIKA MPYA TAMASHA LA WASANIII WA FILAMU DAR LIVE KESHO

MKALI wa miondoko ya muziki wa asili nchini, Vitalis Maembne ni miongoni mwa wasanii wa muzi watakaosindikiza tamasha maalum la wasanii wa filamulitakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo lenye lengo la kukusanya fedha zaidi ya milioni 60 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya shirikisho la filamu tanzania (TAFF) ambapo Maembe aliyepata kutamba na singo ya 'Sumu ya Teja' pia kutakuwa na wasnii wengine kibao wakiwemo Afande Sele, Tundaman, Hemed, Kitale, Shilole, Twanga Pepeta ambapo kiingilio ni sh 15,000 kwa viti maalum na sh 7,000 kwa viti vya kawaida jhuku watoto watalipa sh 2,000.