TFF KUJADILI UCHAGUZI LEO
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board). 
Wanachama wa TFF (vyama vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya Rukwa na Katavi inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu. Kwa upande wa vyama shiriki ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha (TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA), Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo (TASMA). 

Vilevile Kamati ya Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.