TENGA BADO ANANAFASI YA KUGOMBEA URAIS TFF

KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba hakuna kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye katika ya Shirikisho hilo.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa taarifa kwamba rais wa sasa wa TFF Leodger Tenga (Pichani) hapaswi kuwania tena uongozi kutokana na kuongoza kwa vipindi viwili.Uchaguzi wa  Shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam, huzu zoezi la utoaji fomu likitatarjiwa kuanza keshokutwa.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyatto amesema jana kwamba kigezo cha kutogombea ni umri wa chini ya miaka 25 na zaidi ya miaka 75.
Nafasi zitakazowqaniwa ni pamoja na Rais, Makamu wa Raisi na wajumbe 13 wa kamati ya Utendaji.