TBL YAZIKABIDHI VIFAA SIMBA NA YANGA



 Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe akimkabishi jezi ya kipa, ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga kama sehemu ya udhamini wa klabu hiyo pamoja na mahasimu wao Yanga kwa ajili ya ushiriki wao wa mzunguko wa pili wa ligi kuu bara utakaoanza keshokutwa.



Kavishe akimkabidhi vifaa katibu mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako

PRESS RELEASE
24/1/2013

Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya awamu ya pili ya msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii. 
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Bila shaka Simba na Yanga ndio klabu kubwa zaidi hapa Tanzania zikiwa kwa pamoja zimeweza kupata mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu na bado zinaendelea kufanya vizuri. Tunajivunia kuweza kuziunga mkono klabu hizi katika jitihada za  kuwania taji la ligi kuu msimu huu. 
Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu. 
Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza majukumu yetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.  kabisa kwani, pamoja na uhusiano huo mzuri na klabu hizi mafanikio makubwa yanatarajiwa katika kuendeleza soka la Tanzania. 
Kavishe alisema kuwa ushirikiano kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu hizo umesimamia katika misingi ya kufanya kazi pamoja, uadilifu na kuendelea kupata mafanikio. “Ushirikiano huu unasaidia kukuza mpira wa Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa. 
Tunachukua nafasi hii kuwashukuru viongozi wa Simba na Yanga walioko hapa, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu. 
“Tunaahidi ushirikiano kwa klabu hizi nzuri na kama tunavyosema kila mara lengo letu ni kufikisha mpira wa Tanzania kwenye ngazi za kimataifa na kuwafikisha mashabiki wa mpira na wapenzi wa Kilimanjaro Premium Lager kwenye kilele cha mafanikio.”

Comments