SIMBA YAJIMEZESHA KWA CHUI WEUSI

MABINGWA wa ligi kuu bara, Simba SC wamejikuta wakiangukia pua usiku huu baada ya kufungwa bao 1-0 ba Black Leopards ya Afrika Kusinim, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ambayo ilirejwea jana kutoka Oman ilipokwenda kupiga kambi ya maandalizi, iliucheza vema mchezo huo lakini iliangushwa na umaliziaji wa wachezaji wake ambao walijikuta wakikosa mabao ya wazi.
Katika mchezo huo, kilio cha Simba kilisababishwa na beki wake,  Hassan Isihaka aliyejifunga katika  harakati za kutaka kuokoa mpira uliokuwa umetokana na krosi ya mchezaji wa Leopards.
 Leopard iliyotua nchini wiki iliyopita awali ilicheza mechi za kirafiki na Yanga na kufungwa zote ambapo ilianza kutandikwa mabao 3-2 katika Uwanja wa Taifa kabla ya jana kutandikwa mabao 2-1 waliporudiana kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.