SAJUKI AAGA DUNIA

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUN, hivi ndivyo waislam wanavyopaswa kusema unapotokea msiba. Juma Kilowoko “Sajuki”, hatunae tena, amefariki leo afajiri saa 12.
Sajuki amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja.
Sajuki (kulia) akiwa na mkewe, Wastara enzi za uhai wake
Imekuwa ngumu sana kuamini kuwa Sajuki amefariki kutokana na ukweli kuwa mara kadhaa msanii huyo amezushiwa kifo, lakini hatimaye sasa Mungu amempenda zaidi Sajuki.
Marehemu Juma Kilowoko "Sajuki"
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Mohameid Said aliyekuwa analala na marehemu hospitalini hapo, hali ya Sajuki ilibadilika ghafla na kufariki alfajiri ya leo.
Mohamed ameimbia Saluti5 kuwa msiba utakuwa Tabata Bima nyumbani kwa marehemu, lakini akaongeza kuwa bado ni mapema mno kueleza Sajuki atazikwa lini na wapi.
“Kwa bahati nzuri Baba na Mama wapo hapa Dar, watatoa uamuzi baadae kama marehemu atazikwa Dar au Songea” alisema Mohamed katika maongezi yake na Saluti5.
Songea ni nyumbani kwa kina Sajuki na ndipo wanapoishi wazazi wake.