MCHUNGAJI DANIEL NA HOYCE MBOWE WANAWAALIKA KWENYE IBADA YA PILI YA KISWAHILI ITAKAYONYIKA BONN: UJERUMANI

Mchungaji Daniel na Hoyce Mbowe, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika Jumapili hii tarehe 13.01.2013 .
Muda wa Ibada: Saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours).
Mahali: Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn
Anuani: Franz-Bücheler-Straße 10
53129 Bonn
Ibada hii ya Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.
Mawasiliano: dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com
Wote mnakaribishwa: Karibuni tumwabudu na tumsifu Mungu wetu.
Maelezo ya Picha
Iicha ya kwanza : Baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya Ambassador of Christ wakiimba katika ibada ya kwanza mwezi uliopita.
Picha ya pili: Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada ya kwanza wakibadilishana mawazo.