MAKOCHA WA SOKA KUCHAGUANA JANUARI 19


WAKATI uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA) ukitarajiwa kufanyika Januari 19 kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, wagombea watano  tu ndio watakaochuana kwenye  nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura amesema leo kwamba maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yanakwenda vema. 
Alisema alisema mkutano huo wa uchaguzi kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo utatanguliwa na mkutano mkuu wa Tafca, huku akitoa wito kwa vyama vyote vya mikoa vinatakiwa kuwasilisha majina ya viongozi waliochaguliwa katika mikoa yao kwa kamati ya uchaguzi kabla ya Januari 17. 
Wambura amewataja waliojitosa kuwania uongozi katika chama hicho ni pamoja na Oscar Korosso na Lister (Uenyekiti), Michael Bundala  (makamu Mwenyekiti), Wilfred Kidau na Lugora wanaowania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. 
Aidha, Wambura aliongeza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa wadau walioomba kuwania nafasi za Uhazini na Katibu Mkuu, nafasi hizo zitajazwa katika mkutano utakaoitishwa baadaye.