MAJINA YA WAGOMBEA TFF HADHARANI JIONI HII


Baada ya kupitia fomu za waombaji uongozi TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF leo saa 10 kamili jioni itabandika kwenye ubao wa matangazo wa TFF majina ya waombaji ili kutoa fursa kwa kipindi cha pingamizi. Mwisho wa kupokea pingamizi dhidi ya waombaji uongozi ni tarehe 26/01/2013 saa 10 kamili alasiri.
 
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)