HASSANOO AJAZA FOMU ZA KUWANIA UONGOZI TFF AKIWA LUPANGO

MWENYEKITI wa Chama cha soka mkoa wa Pwani (COREFA) Hassan Othaman Hassananoo jana ambaye yupo gerezani akikabiliwa na kkesi ya uhujumu uchumi, amejitosa kuwania ujumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) akiwakilisha mikoa ya Pwanmi Na Morogoro.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya COREFA Masau Bwire ndiye aliyekwenda kumchukulia fomu Hassanoo na kumpelekea kuzijaza kabla kuzirejesha TFF na kusubiri mchakato mwingine.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu ambapo mbali na Hassanoo wengine walioomba kugombea katika kanda hiyo ni _Farid Nahdi, Riziki Majala na Twahili Njoki