GAPCO YADHAMINI TENA MBIO ZA NUSU MARATHON KWA WALEMAVU


Kwa mara nyingine tena kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania imetambua umuhimu wa wanariadha wenye ulemavu kwa kuwapa fursa ya kushiriki kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 kwa kudhamini mbio ya nusu marathon kwa ajili ya walemavu itakayojulikana kama GAPCO GAPCO 21km Disabled Half Marathon.
Mkuu wa Mauzo na Maskoko wa GAPCO, Ben Temu amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa “Ushiriki wa wanariadha wenye ulemavu unaleta msisimko mpya kwenye Kilimanjaro Marathon kwa mara nyingine tena. Kukimbia marathon kunaendana na mambo ambayo GAPCO inayaamini katika shughuli zake za kila siku – mtazamo chanya, kipaumbele katika kujiamini na azma ya kusonga mbele”.
“Ushiriki wa walemavu ni ushaidi kwamba watu wenye ulemavu sio tu kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa bali pia inadhiirisha kuwa wana uwezo wa kutimiza jukumu lolote kwa ufanisi wa hali ya juu. Kama wadhamini tunahimiza jamii nzima pamoja na makampuni mengine yajitolee kudhamini walemavu waweze kushiriki Kilimanjaro Marathon katika siku zijazo,” alisema.
Mbio za hizo zitakuwa na sehemu tatu ambazo ni kiti cha magurumu (wheelchair), baiskeli ya miguu mitatu, na walemavu wanaokimbia. Washindi watajipatia zawadi nono ambazo jumla yake ni zaidi ya shilingi milioni 3.
GAPCO ina nia thabiti ya kuwasaidia wanariadha walemavu ili waweze kutimiza ndoto zao na kuthibitisha kwamba wanaweza.
Kwa mujibu wa John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waadaaji wa mbio hizo, Kilimanjaro Marathon ni kati yam bio zenye mvuto zaidi duniani kutokana na kwamba zinafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro na ndio maana huvutia washiriki kutoka nchi zaidi ya 40 kila mwaka. Mbio hazivutii wanariadha peke yao bali pia watalii ambao huchangia pato la taifa”, alisema.

Comments