DESTINY'S CHILD WAREJEA UPYA KWENYE GAMENEW YORK, Marekani
KUNDI la muziki lilowahi kutamba hapo nyuma la Destiny's Child limetangaza kurejea upya likiwa pamoja ambako wanatarajia kuachia albamu yao mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Nuclear’.
Kundi hilo la muziki wa R&B lilitoa taarifa hiyo juzi baada ya kukaa kimya tangu mwaka 2004 ambako ndipo walitoa albamu yao ya mwisho na kila mmoja kutawanyika na kufanya kazi binafsi.
Albamu ya ‘Nuclear’ inatarajiwa kuwa na nyimbo 13 ambazo ziliwahi kutamba hapo nyuma kama vile ‘Emotion’ na ‘Cater 2 U’ na baadhi ya kazi mpya ambazo zinatarajiwa kuwemo ni pamoja na ‘Love Songs’ inayotarajiwa kutoka Januari 29.
Kazi hiyo ya ‘Nuclear’ imetengenezwa chini ya utayarishaji wa Pharrell, akiwa ameshirikiana na mwimbaji Michelle Williams.
Destiny's Child, inaundwa na waimbaji kama vile Williams, Beyonce Knowles na Kelly Rowland ambao walifanikiwa kutikisa ile mbaya katika anga za muziki na kuushtua ulimwengu lakini baadaye kukaibuka malalamiko kutoka kwa weaimbaji wengine wakilaumu kwamba nafasi kubwa anakuwa anapewa mwimbaji Beyonce kwa sababu mkurugenzi wao alikuwa baba mzazi wa mwimbaji huyo.