CAF YAIPIGA JEKI TFF


SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) limetoa ufadhili kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika kurabati kituo chake cha michezo kilichopo Karume jijini Dar es Salaam.
 Ufadhili huo ni sehemu ya mpango wa kusaidia wanachama wake katika dhima nzima ya kuchangia maendeleo ya soka ambapo utahusisha kukarabati maeneo mbalimbali ya mpango huo ikiwemo uwanja na hosteli zilizopo Karume.
Tayari zimeshatangaza tenda kwa makampuni mbalimbali ili kujitokeza kwa ajili ya kuendesha mradi huo kabla ya bodi husika kukaa na kuteua kampuni itakayofanya ukarabati huo.