BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AKUTANA NA WACHEZAJI WA SEATLLE SOUNDERS KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na ujumbe wa wachezaji na waandishi wa habari kutoka timu ya seattle Sounders ya Canada wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB kwenye hoteli ya serena jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya ugeni huo, Bodi ya Utalii ilisaini mkataba wa kutangaza utalii wa Tanzania katika kiwanja cha timu hiyo katika ziara iliyofanywa na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki nchini humo katika msafara huo unaoongozwa na mchezaji wa mpira wa American Football Kevin Griffin ambaye pia ni Fan Development Marketing wa Sunders FC, wachezaji hao walitembelea mbuga za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mbuga ya Tarangire ambapo walipata muda wa kujionea vivutio vilivyomo katika hifadhi hizo na kupiga pichaBalozi Khamis Kagasheki akimsikiliza mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi ambaye ndiye mwenyeji wa wageni hao wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam jana, kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu.

Ugeni huo ukipata chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jana usiku kutoka kulia ni Kevin Griffin mchezaji wa mpira wa American Footballn Kasey Keller mchezaji maarufu wa mpira wa miguu vilabu mbalimbali Ulaya na Marekani na mchezaji wa timu ya Taifa ya MarekaniKristen Addings kutoka Taasisi ya Washington Global Hearthna David Glass Mtaalam Video na Majarida

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo kushoto ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dr. Aloyce Nzuki akizungumza na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo wakati wa hafla hiyo, katikati ni Mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi.

Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Mh. Waziri Balozi Khamis Kagasheki na wageni kutoka Seatlle Sounders kwa ajili ya kujitambulisha na kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na bodi hiyo.

Kevin Griffin ambaye ndiyo kiongozi wa msafara huo akimshukuru Mh Waziri na Uongozi wa Bodi ya Utalii TTB kwa ushirikiano waliouanzisha katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini Canada.

Kasey Keller akizungumza katika hafla hiyo.

Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya Saa Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya saa Ibrahim Musa Mkurugenzi wa Utalii katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mh. Waziri Balozi Khamis Kagashiki akiongozana na Mchezaji wa Seatlle Sounders Marc Burch kuelekea katika meza ya chakula.


Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na waandishi wa habari kutoka Seatlle Sounders nchini Canada pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii.