AROBAINI WARIPOTI KAMBI YA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013


Jumla ya warembo arobaini kati ya sitini wa Miss Utalii Tanzania kutoka mikoa yote ya Tanzania.tayali wameripoti kambini leo,kuanza kambi Taifa ya siku 21  kuanzia leo. Kambi hiyo mwaka huu iko katika Hoteli ya Ikondelelo Lodge iliyoko Kibamba Dar es Salaam. 
Warembo walio ripoti kambini hadi sasa ni kutoka mikoa ya Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1(Elline Bwire),  Kagera2 (Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda),  Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Tanga (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange). 
Warembo wote wakiwa kambini,watapewa mafunzo na semina mbalimbali kuhusiana na Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Afya ya Jamii, Elimu ya Jamii, Wanyama Pori, Mazingira, Madini,Ulinzi Shirikishi n.k, chini ya jopo la wakufunzi la mashindano haya wakiongozwa na mkufunzi mkuu (Chief Choreographer) Erasato Gideon, pamoja na Mkufunzi Mkuu wa Ngoma za Asili Mariam A. Kweji toka Kaole Sanaa Group,Mkufunzi wa Miziki na Dansi la Asuku Che Mundugwao,wakufunzi wa minato na miondoko ya Urembo na Mitindo Caroline Y. Mrosso na Evamary Gamba .

Comments