50 CENT ASHINDA KESI


NEW YORK, Marekani
RAPA 50 Cent amefanikiwa kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kuiba wazo la mtu katika utengenezaji wa albamu na filamu ya jina ‘Before I Self Destruct’.
Kesi hiyo iliyokuwa imeungulia na Shadrach Winstead ayekuwa akidai kwamba msanii huyo aliiba wazo lake alilokuwa amelitoa kwenye kitabu chake kinachojulikana kama ‘The Preachers Son – But the Streets Turned Me into a Gangster’.
Alikuwa akidai kuwa 50 aliamua kuchukua hadithi yake na kuiweka katika muziki na filamu kutoka katika kitabu hicho.
Madai hayo ya Winstead yalitupwa na jaji wa mahakama ya mjini hapa, Stanley Chesler na kudaiwa kwamba hayakuwa na mashiko