ZANZIBAR HEROES NAO WATINGA NUSU FAINALI CHALENJI

Wachezaji wa Zanzibar wakiwa wamembeba kipa wao, Mwadini Ally baada ya kupangua mkwaju mmoja wa penalti, na kuiwezesha timu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 5-4 kwenye Uwanja wa Lugogo, mjini Kampala, Uganda jioni hii. Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi.(picha na BinZubeiry blog)