YANGA YAPIGWA KIDUDE NA TUSKER


Nizar Khalfan wa Yanga kushoto akimtoka beki wa Tusker leo. Habari picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog
 MABINGWA wa Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki.
Huo ulikuwa mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.  
Hadi mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo, ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja ametoa sare.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda, Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC; George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,