WAREMBO MISS UTALII KAMBINI JUMATANO
 Huu ni ukumbi ambao utatumika kwa ajili ya Mazoezi   pamoja na shughuli mbalimbali.
 Hii ni Lodge Maalum ambayo Warembo watafikia
Hivi ni viunga ambavyo warembo watapata nafasi ya kupumzika pindi watakapo kuwa wamechoka na kazi pamoja na mambo mbalimbali
Jumla ya warembo Sitini (60)  kutoka nchi nzima na vyuo vikuu  watakao shiriki fainali za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 wanatarajia kuanza kambi Rasmi Tarehe 19.12.2012 katika hoteli ya kitalii ya Ikondolelo Lodge iliyopo kibamba Dar es salaam.
Wakiwa katika kambi hiyi ya siku ishirini na moja , warembo hao watashindana kuwania taji la taifa la Miss Utalii Tanzania , na tuzo mbalimbali za kijamii kitalii kitamaduni na kiuchumi. Zikiwemo tuzo za Mazingira, utaluii wa ndani, wanyama pori,hifadhi za Bahari, Mitindo, urembo, maziwa makuu, SADEC, Afrika Mashariki, umoja wa Afrika  Afya ya jamii, Jinsia wanawake na watoto, Rushwa, uwekezaji, Madawa ya kulevya, mazao ya biashara, madini , uchukuzi na Miundombinu mbalimbali ya utalii.
Washiriki pia watajifunza stadi mbalimbali za maiusha , Mbinu za utangazaji utalii na bidhaa mbalimbali za Tanzania, Pia mbinu za kjuhamasisha kampeni dhidi ya uharibufu wa mazingira, tanamaduni kongwe na potefu, kupenda kutumia huduma za Tanzania ( Madre in Tanzania), uvuvi haramu, amna uwindaji haramu.
Washindi wa fainali hizo za taifa watawakirisha fainali mbalimbali za kitaifa na kimataifa yakiwemo ya, Miss Tourism world, Miss Tourism HeritageWorld Miss Tourism University World, Miss Tourism Uniterd Nation,International Miss tourism World, Miss Global International.