Skip to main content

UNIQUE MODELS 2012 KUPATIKANA DESEMBA 28@MAISHA CLUB


Fainali za kumsaka Unique model of the year 2012 katika shindano la Unique model zitafanyika tarehe 28 desemba mwaka huu katika ukumbi wa New Maisha club uliopo Oyterbay jijini Dar.
Fainali hizi zitasindikizwa na burudani ya toka bendi ya Mashujaa ikiongozwa na Chaz Baba,mfalme Costa Siboka atatoa burudani ya vionjo vya nyimbo za asili na upande wa bongo flava kutakuwa na suprize yakufa mtu,pia kwa mara kwanza jukwaani msanii Bshop atatoa burudani ya aina yake.
Jumla ya washiriki 12 wanategemewa kupanda jukwaani siku hiyo ikiwa zimebaki siku chache kabla ya fainali hizo homa ya nani atachukua taji hilo linazidi kupanda baada ya wadau wa mitindo nchini Tanzania kutupia jicho zaidi katika shindano hili lenye msisimuko wa aina yake.
 Wapenzi wa burudani na tasnia ya mitindo wameombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani atavishwa taji hilo ambalo limekua gumzo jijini Dar kutokana na ushindani mkubwa kati ya washiki hao 12.

Baada ya shindano kumalizika burudani ya wasanii wa bongo flava itaendelea mpaka alfajiri kwani tumepania kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani siku hiyo ambapo uhondo huowote  utakuwa ni kwa Tsh 15,000/= tu.
Red carpet kwa mastaa na watu wote watakaopendeza siku hiyo itakuepo,pia kutakua na kitu kipya kabisa katika matukio ya mitindo nchini Tnzania.