TWANGA, DIAMOND MUSICA WAFUNIKA TUSKER CARNIVAL MOSHI

Bendi  za Musiki wa Dansi zenye miondoko ya Ndombolo ya Solo, za Twanga Pepeta na Diamond Musica usiku wa kumkia jana zilifunika na kukonga nyoyo za wapenzi wa Muziki wa Dansi mjini Moshi wakati wakali hao wawili walipotumbuiza katika Tamasha kubwa la Burudani la Tusker Carnival lililofanyika katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Walikuwa ni Diamond Musica ndio walioanza kushambulia Jukwaa hilo la Tusker Carnival mishale ya saa mbili usilku hadi sita kasorobo walipo wapisha Wakongwe wa Burudani na Wabishi wa mjini Twanga Pepeta ambao walitikisa vilivyo Mji wa Moshi. 
Tamasha hilo la Tusker Carnival lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadae kupigwa jijini Mwanza huku Nguli wa Mziki wa dansi Koffi Antonio Olomide akiongoza mashambulizi. Leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka kwa Mapacha wa tatu na kundi la Extra Bongo chini ya Ali Choki.
 Kijana wa Mjini Moshi ambaye anakula Maisha jijini Dar es Salaam akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha lka Tusker Carnival.
 Mamaa Luwiza Mbutu akifanya makamuzi
 Wacheza show wa Twanga Pepeta wakifanya makeke
 Hawa ni Diamond Musica wakishambulia jukwaa la Tusker Carnival
 Wadau wa Father Kidevu Blog, kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti tawi la Mjini Moshi nao walikuwepo ndani ya Viwanja vya Ushirika Mjini Moshi na hapa wakishow LOVE ndani ya Tusker Carnival.
 Wadau wakila Bata huku wakishushia na Tusker Baridi, ilikuwa ni burudani na makulaji katika tamasha la Tusker Carnival.
 Wadau wa Mjini Moshi nao walikuwepo uwanjanai hapo.
 Watu waliyarudi magoma kama kawaida
 Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta akifanya vituko vyake katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika mtu nyomi zikifuatilia Burudani kutoka Tusker Carnival

Comments