TIMU YA WABUNGE WA TZ YABANJUA WENZAO KENYA 51-25

Timu ya Tanzania
 Tanzania yaendeleza ubabe wa kwa timu za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya timu ya mpira wa kikapu wananwake kuinyanyasa Kenya Bunge Sports Club kwa mabao 51-25. Wakati huohuo, timu ya wanaume imeedelea kutoa adhabu kali leo ikiwa ni zamu ya Rwanda ambapo hadi kipenga cha mwisho Tanzania 6 Rwanda 0. Jana Kenya ilibamizwa bao 5-0
                                                                          Timu ya Kenya

Tanzania Bunge Sc

Tanzania Bunge Sports Club Football imefanya maajabu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi jana kwa kuwabamizwa wenyeji wao timu ya Kenya Bunge Sports Club Football mabao 5-0e katika michezo ya mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Nairobi. Mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi tarehe 7 Disemba na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo 
Katika mashindano haya ambayo hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Burundi haikushiriki.Chini ya ukufunzi wa Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala (Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe. Joshua Nassari. (Na Prosper Minja)