OKWI AELEKEA 'KIBLA' MSIMBAZI, AJIFUNGA MIAKA MIWILI


HATIMAYE mshambulaiji wa kimataifa wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea timu hiyo.
Awali kulikuwa na hatihati ya Simba kumkosa mchezaji huyo ambaye alitaka dola 40,000 ili aweze kusaini mkataba mpya, kabla mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe kuokoa jahazi. 
Zoezi la kusaini mkataba huo lilifanyika jana  usiku nchini Uganda ambapo zoezi hilo limesimamiwa na mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Ade Rage pamoja Hans Poppe.