MSONDO, SIKINDE USO KWA USO EQUATOR GRILL, SIKU YA KRISMAS


                                              Msondo Ngoma wakiwa kazini
                                               Sikinde Ngoma ya Ukae wakishoo love kwa wadau

Na Mwandishi Wetu
Baada ya kila mmoja kupewa vyombo vipya na Konyagi, bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  zitapambana siku ya Krismasi katika ukumbi wa Equator Grill, Temeke.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2012.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2012.
Mratibu huyo alisema bendi hizo zitapiga jukuwaa moja lakini kila moja atatumia vyombo vyake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itatumia muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa pambano la aina yake ukizingatia kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kwa bendi hizo kupambana siku ya Krismasi tangu zianzishwe. Mwaka jana zilipambana katika TCC Club Chang’ombe,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo itaanza saa tisa alasiri hadi liamba.