MSONDO NGOMA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 KIVULE

WAKONGWE wa muziki Tanzania, Msondo Ngoma imeandaa onesho la kuukaribisha mwaka mpya 2013 katika ukumbi wa Vegetable Garden Pub, uliopo Kivule, Ilala Dar es Salaam.
Meneja wa Msondo Ngoma, Athumani Kibiriti alisema katika onesho hilo nyimbo mpya ambazo zimetungwa kuukaribisha mwaka mpya zitaimbwa.
Alisema Msondo Ngoma ambayo imesheheni wanamuziki wenye uzoefu mkubwa wataongozwa na Muhidin Gurumo, Shaaban Dede, Roman Mng'ande 'Romario',Said Mabera na Hassan TX Moshi William.
Naye mwanamuziki wa bendi hiyo Roman Mng'ande alisema ameandaa shoo mpya ambayo  itaanza kuonekana kesho na kuwaahidi mashabiki kupata burudani itakayowakonga nyoyo za mashabiki.
Mkurugenzi wa ukumbi wa Vegetable Pub, Anicety Mkwaya alisema zawadi zitatolewa kwa wanamuziki na mashabiki watakaocheza msondo ngoma halisi.