MBWANA MATUMLA KUZIDUNDA NA MKENYA, SIKU YA KRISMAS

INAPENDA KUWAARIFU KWAMBA HAPO TAREHE 25-12-2012 [SIKUKUU YA CHRITSMAS] KATIKA UKUMBI MAARUFU WA BURUDANI WA DAR-LIVE ,ULIOKO MABGALA WILAYA YA TEMEKE MKOANI DARESALAAM , KUTAFANYIKA PAMBANO KUBWA LA NGUMI ZA KULIPWA LA KIMATAIFA ,KATI YA BONDIA BINGWA WA ZAMANI WA KIMATAIFA ALIYEKUWA ANATAMBULIWA NA CHAMA CHA NGUMI ZAM KULIPWA DUNIANI [WBA] ,MBWANA MATUMLA ATAPANDA ULINGONI KUPAMBANA NA MKENYA DAVID CHARANGA .


PAMBANO HILO LITAKUWA LA UZITO WA KILO 55.3 [SUPER BANTAM ,NA LITAKUWA LA RAUNDI NANE [8]

TAYARI BONDIA HUYO MTANZANIA AMESHASAINI MKATABA WA KUCHEZA PAMBANO HILO AMBALO LINAANDALIWA  NA KAMPUNI YA GLOBAL PUBLISHERS AMBAO NI MAARUFU SANA KWA KUANDAA MATAMSHA MABLIMBALI YA BURUDANI YAKIWEMO YA KIMATAIFA.

PIA SIKU HIYO BONDIA MAARUFU  KATIKA UZITO WA  KILO 76-5 [UPER MIDDLE] MADA MAUGO ATAPANDA ULINGONI KUZUIPIGA NA BONDIA MGANDA YIGA JUMA KATIKA PAMBANO LA RAUNDI SITA [SITA]


NAYE BONDIA KUTOKA MKOANI IRINGA CHUPAKI CHIPINDI ATAZIPIGA NA BONDIA KUTOKA JIJINI DAR-ES-SALAAM BAHATI MWAFEL KATIKA UZITO WA CRUISER -KILO 86.


ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO-LIMITED] IMESHATOWA KIBALI CHA PAMBANO HILO NA INAWATAKA MABONDIA WOTE WANAOHUSIKA NA PAMBANO HILI KUTOWA USHIRIKIANO WA DHATI KWA WAANDAAJI WA PAMBANO HILI KAMA MIKATABA INAVYOELEZA.


                          IMELETWA KENU NAMI
                 YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA-USTAADH
                       RAIS -TPBO  -LIMITED