KHADIJA KOPA NA TOT TAARAB KULA KRISMAS KIVULE

MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa na kundi lake cha Tanzania One Theatre (TOT)leo (Jumanne)kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.

Akizungumza jana, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kitamba na nyimbo kemkem za taarab zinazotingisha katika miundoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake katika eneo hilo kwenye sikukuu hiyo.

Alisema TOT taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.

Mkurugenzi wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakacheza taarab vizuri na watakaovaa vizuri.

Alisema burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambako Januari 29 bendi ya Msondo Ngoma itatoa burudami katika ukumbi huo.