JOSEPH OWINO AREJEA SIMBA SC, UHURU SELEMAN AANZA KAZI AZAM FC                                                           
                                      Uhuru Suleiman
Hatimaye beki mahiri wa azam fc Joseph amerejea ktk klabu yake ya zaman,simba sc. 
 Aidha kiungo mahiri wa simba,uhuru suleiman naye ametua azam fc baada ya timu hizo kubadilishana wachezaji.    
Habari za uhakika kutoka Azam zinaeleza kwamba zoezi hilo limekamilika baada ya kukamilisha mchakato na tayari uhuru ameshaanza mazoezi na wenzake. 
 Kiongozi huyo aliongeza kuwa owino ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni kwao kenya ätajiunga na wekundu hao pindi atakaporejea nchini.   
Ikumbukwe kuwa owino alipata Kuichezea simba miaka miaka miwili iliyopita kabla ya kuumia goti na kwenda kujitibia kwao ndipo azam ilipomsajili na kumpeleka india kwa matibabu zaidi.    
Katika hatua nyingine simba ipo katika mazungumzo na azam fc ili kuweza kumchukua kwa mkopo nyota wake,agrey morris ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana kwa madai ya kuihujumu timu hiyo.   
Simba ambayo ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara ikiwa nafasi ya tatu kwsa sasa ipo katika kuimarisha kikosi chake