FAINALI UNIQUE MODEL 2012 LEO@NEW MAISHA CLUB


FAINALI za shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ kwa mwaka 2012 zinatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa New Maisha Club uliopo Oyesterbay jijini Dar es Salaam  ambapo warembo 12 watachuana kuwania taji hilo. 
Mkurugenzi wa Unique Entertainment inayoandaa shindano hilo, Methuselah Magese alisema kwamba maandalizi ya shindano hilo yamekamilika, hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali hizo. 
Alisema  shindano hili linatarajiwa kuwa na ushi ndani mkubwa kutokana na washiriki wake kuwa na viwango vya hali ya juu hali itakayowapa mtihani mkubwa majaji katika maamuzi yao. 
Magese aliwataja washiriki hao ni Janecy Maluli,Judith Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling Godfrey,Amina Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib ambao walikuwa kambini kwenye hoteli ya Lamada kwa wiki mbili chini ukufunzi wa Wancy Nells kwa upande wa miondoko na Denis Lucas kwa upande wa shoo. 
Aidha, Magesa alisema tayari Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limeteuwa majina matatu ya majaji  watakaoshiriki katika kumchagua mshindi wa taji hilo linoloshikiliwa na Asia Dachi kuwa ni wabunifu  Asia  Idarous Khamsini,Gymkhana Hilall  ‘paka wear’ na Martin Kadinda ‘Singo Button’. 
Shindano hilo limedhaminiwa na Giraffe Ocean view Totel,Kitwe General Traders,Sophanaa Investment ltd,Dtv,88.4 clouds fm,Magazeti ya  Tanzania Daima na Kiu,Mashujaa Investment Ltd,Blogu za Michuzi,jiachie,Mtaa kwa Mtaa, Unique Entertainment,, Lamada Apartments & Hotel, Fabak fashions,Genessis Health Center na Yung don Records,Paka Wear na Mtoko Design litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa ikiongozwa na rapa maarufu Chalz Baba, msanii wa ngoma za asili toka kwa Costa Siboka na msanii wa bongo flava B-shop.