BASENA AREJESHWA SIMBA SC, WACHEZAJI WASHEREHEKEA KRISMAS

MABINGWA wa ligi kuu ya Vodacom Simba Sc, wamemreja kundini kocha wao wa zamani Mganda, Moses Basena (pichani).
Basena ambaye alitimuliwa Simba SC na mikoba yake kurithiwa na Mserbia Milovan Cirkovic anarejea Simba kama Kocha msaidizi ambapo atakuwa chini ya Mfaransa, Patrick Liewang.
Aidha, kikosi cha Simba ambacho kilianza mazoezi hivi karibuni chini ya kocha wa muda, Jamhuri Kihwelo 'Julio' kimekwenda mapumziko kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi ambapo mazoezi yataendelea Alhamis.