AZAM FC KWENDA CONGO DRC KESHO

KLABU ya soka ya Azam Fc inaondoka nchini kesho kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kushiriki mashindano maalumu nchini humo ambayo yanatarajiwa kuanza jumamosi na kushirikisha timu kadhaa.
Azam ambayo itaondoka na kikosi chake chote inatarajiwa kutumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom utakaoanza mwezi Januari pamoja na michuano ya kimataifa.