YANGA KUPIGA KAMBI UTURUKI



Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdallah Binkleb akizungumza na waandishi wa habari leo, kulia ni kocha mkuu wa Yanga, Ernie Brandts


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu bara, Klabu ya soka ya soka ya Yanga inatarajia  kupoga kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdallah Binklen ameiambia Sports Lady leo kwamba, ziata hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na  Februari 25, 2013.
Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na timu hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.
Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.
Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 wakiwemo kipa, Yusuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.
Katika hatua nyingine, Binkleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya mwenyekiti Yusuf Manji kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Kagame, kufanmya vema katika mzunguko wa kwanza wa ligi ambao ulimalizika kwa timu kuongoza, timu kuweka kambi nchini Rwanda, pamoja na nyota wake Said Bahanuzi kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Kagame.

Comments