WAREMBO MISS EAST AFRICA KUANZA KUWASILI KESHO

  •  
Warembo wanaoshiriki mashindano ya Miss East Africa 2012 wanatarajiwa kuanza kuwasili kesho jijini Dar es salaam wakitokea katika Nchi mbalimbali tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayo fanyika tarehe 07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
wakati huo huo Mtangazaji mashuhuri wa Mnet na ambae amewahi kuwa mshindi wa Big Brother Africa, Gaetano Kagwa anayeishi Afrika Kusini ndiye atakaekuwa MC wa mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika jijini dar es salaam
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius na warembo mbalimbali wa Afrika mashariki walioshindana katika Nchi mbalimbali za Ulaya
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam

Comments