UONGOZI SIMBA WAMUOMBA RADHI KASEJA, KIKOSI KWENDA HOLIDAY ULAYA


KATIKA kuhakikisha  ari ya wachezaji inarudi kama ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa klabu ya Simba una mpango wa kuipeleka timu nje ya nchi ili kuwapa muda wachezaji wa kusahau yaliyopita na kujipanga vema kwa mzunguko wa pili. 
Aidha, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, umemuomba radhi kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na kudhalilishwa na baadhi ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha katika michezo yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza. 
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba  kudhalilishwa kwa Kaseja si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi kama binadamu mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo. 
“Tuache kudhalilisha wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata kidogo…kila mtu anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama hatutaki kufungwa tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage

Comments