TUZO YA MWANASOKA BORA KUTOLEWA DESEMBA 30Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka  zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika sehemu (venue) itatangazwa baadaye.

Mchakato wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.

Kwa sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na  mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.

Aidha kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya baadaye baada ya kustaafu.

Sababu za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.

Kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.

Semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na  20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na  utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa wachezaji pekee.

Tuzo za aina hii ni za kwanza kufanyika nchini Tanzania ambapo mshindi wa tunzo hiyo anatarajiwa kuopata tuzo, fedha taslim, medali na cheti.

Imetolewa na
Ahadi Kakore- Mratibu
Novemba 20 2012