SHIRIKISHO la soka Tanzania
(TFF) pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, wanatarajiwa
kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kuzungumzia
mustakabali mzima wa suala la makato katika michezo mbalimbali.
Hatua hiyo inafuatia TRA
kuzifunga akaunti za udhamini wa ligi hiyo kama
shinikizo kwa TFF kulipa makato ya kodi
kwenye mishahara ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ tangu kipindi cha kocha Mbrazil
Marcio Maximo kwa madai kwamba imekuwa haikatwi kodi za mishahara ya makocha na
hivyo kufikia sh milioni 157,407.968.00.
Rais wa TFF, Leodger Tenga
amesema leo walichokifanya TRA ni jambo la heri kwani
kinaonyesha majukumu ya Serikali katika soka.
Alisema ukaribu uliopo sasa
baina ya Serikali chini ya Rais Kikwete na soka ni mkubwa kutokana na ukweli
kwamba inachangia kwa kiasi kikubwa
kulipa mishahara ya makocha wa timu za Taifa.
Alisema suala hilo linahitaji mazungumzo
baina ya pande hizo ili kuweza kulipatia ufumbuzi na hakuna haja ya kuilaumu
TRA kwa sababu inafuata taratibu zilinazostahili kwa mujibu wa kanuni.
“Hawana njia nyingine ya
kufanya hivyo ufumbuzi ni sisi ni kukutana na Wizara na TRA ili kulizungumza
hili na katika siku mbili hizi tunarajiwa kukutana,”alisema
Tenga aliongeza kuwa TFF
haina uwezo wa kulipa fedha hizo na kwamba hela zilizochuliwa si za Shirikisho hilo bali ni za ligi kuu
Bara ambazo zimetolewa na wadhamini wake, kampuni ya simu za mkononi,Vodacom
kwa maelekezo maalum.
“Ni jambo nyeti na lazima
lifanyiwe kazi, hatuwezi kumlamu mtu na nimatumaini tutakapoketi pamoja
tutapata ufumbuzi,”alisema.
Aidha, Tenga alisema
wanatarajia kuzungumzia suala la makato ya michezo mbalimbali ambayo yamekuwa
yakilalamikiwa na vilabu kwa muda mrefu.
“Changamoto za namna hiyo
tumekuwa tukizifanyia kazi kwa muda mrefu na ndiyo maana tangu mwaka 2005
asilimia ya makato ya TFF imekuwa ikipunguzwa, nadhani ni kuendelea kuwa na
subira.
Comments
Post a Comment