TFF YAPOTEZEA VIJEBA WA CONGO BRAZAVILLE, YAWATAKA SERENGEI KUPAMBANA KIUME


RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga amewataka wachezaji wa timu hiyo kuachana na fikra ya kuwa wapinzania wao, Congo Brazaville inaundwa na wachezaji waliozidi umri ‘Vijeba’ , badala yake vijana hao wajitume ili ushindi upatikane. 
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa malalamiko ya Congo Brazavile kuchezesha Vijeba katika mechi yao ya awali ya kuwania kucheza fainali za Afrika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0. 
Tenga amesema haoni sababu ya kuwakatia rufaa kama ilivyoelezwa awali, kwani tayari walisharipoti kwa kamishna wa mchezo huo na  kama watafanya hivyo itakuwa baadaye. 
Alisema wachezaji hao hawana budi kuelekeza akili zao kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa ugenini mwishoni mwa wiki hii na kuhakikisha wanashinda ili kusonga mbele. 
“Nisingependa hili neno la Vijeba liingie katika akili za hawa watoto ili waende kupambana na kurudi na ushind,”alisema. 
Aidha, Tenga amewapongeza vijana hao kwa ushindi walioupata katika mchezo wao wa awali licha ya kuwa ni finyu na kuwataka kuendelea na moyo wa kujituma ili waweze kufika mbali. 
“Pia TFF inashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yao, sambamba na kamati ya kuisaidia Serengeti kwa mchango wao wa hali na mali,”alisema. 
Katika hatua nyingine, Tenga ametolea ufafanuzi suala la mgawo wa sh mil 1 kati ya mil 23 zilizopatikana katika mchezo wa Serengeti Boys na wenzao wa Congo Brazaville baada ya kamati ya kuisaidia Serengeti ambayo ilichanga milioni 35 kulalamika. 
Tenga alisema mil.35 zilizochangwa na kamati hiyo zilitumika kufidia hasara iliyopatikana katika mchezo huo kwani mchezo unaofanyika katika uwanja wa Taifa na kuingiza chini ya mil.80 ni lazima TFF ibaki na madeni. 
“Ndiyo maana tumekuwa tuklipeleka mechi bndogondogo na zile za vijana katika uwanja wa Uhuru kwa sababu ya gharama za Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na uwanja wa Uhuru kutotumika ndo hatuna dudi kubaki Taifa na matokeo yake ndiyo kama hivyo.”alisema Tenga. 
Tenga aliongeza kwamba, mara nyingi TFF imekuwa ikipata mzigo wa kulipa madeni yanayotokana na hasara za michezo mbalimbali inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa. 
Tenga alisema kwa sasa timu hiyo inatakiwa kuendelea kujengwa kisaikolojia ili iweze kuwa katika hali nzuri na kufanikisha malengo yake ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania. 
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wa Serengeti  Boys kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Congo Brazzavile tayari kwa mchezo huo.

Comments