TFF HAIJAKATA TAMAA NA KINA SAMATTA, ULIMWENGU


                                                                           Samatta
Ulimwengu
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limeandika barua kwa Cgama cha Soka cha  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ili kuwasaidia kuruhusiwa kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza katika klabu ya TP Mazembe ya huko, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu. 
Hatua hiyo inafuatia uongozi wa TP Mazembe chini ya Rais wake Moise Katumbi kugoma kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na timu ya Taifa ya Bara ‘Kilimanjaro Stars’ inayoshiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Uganda.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema jana kwamba wameamua kupitia kwa Chama hicho baada ya TP Mazembe kutowaruhusu nyota hao kwa madai kuwa timu inakabiliwa na michezo kadhaa. 
Alisema kwa sasa timu hiyo haina mashindano yoyote, hivyo ingekuwa vema kuwaruhusu wachezaji hao ili waweze kuisaidia Kili Stars katika hatua ya roibo fainali iwapo itafuzu. 
“Rais wa TFF, (Tenga) alishaongea na uongozi wa TP Mazembe, kabla ya kuongea na rais wa Fay a Congo  walipokutana katika mkutana wa viongozi wa CECAFA, lakini tumeona tutume na barua ili kusisitizia sula hilo,”alisema Osiah. 
Aidha, Osiah alisema anaamini suala hilo litashughuliwa ili wachezaji hao waweze kuruhusiwa kwa sasa kuituymikia timu ya Taifa na pindi Tp Mazembe itakapowahitaji wataenda kuitumikia,”alisema Osiah.

Comments