SHARO MILIONEA KUZIKWA LEO NYUMBANI KWAO TANGA

Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa maigizo na Mziki wa Bongo fleva kufariki zimasamba nchi nzima masaa machache yaliopita.

Kwa mujibu wa Sam Misago.Com ni kwamba amepata uthibitisho kutoka kwa diwani Makame Seif ambaye ni rafiki yake wa karibu sana wa Marehemu Hussen Ramadhani Mkiete maarufu kama Sharo Millionea amepata ajali mida ya saa mbili eneo la maguzoni Tanga na amefariki dunia papo hapo. Polisi wametambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.

Diwani huyu amemfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono. Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule ya Tanga.

Tunamuombea Ndugu yetu SHARO MILLIONEA Apumzike Kwa Amani....