SERENGETI BOYS YATUA SALAMA CONGO BRAZAVILLE, YAAHIDI MAKUBWA KESHO


Timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetua salama mjini Congo Brazaville tayari kwa mchezo wa marudiano na wenyeji utakaopigwa kesho ugenini.
Timu hizo zinakwaana katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo ambapo Serengeti  itashuka dimbani ikiwa mbele kwa bao 1-0 ililolipata katika mchezo wa awali uliopigwa wiki iliyopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Kwa hali hiyo Stars inahitaji kushinda ama sare yoyote ili kuweza kufuzu fainali hizo hizo kwa mara ya kwanza. 
Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah ameiambia Sports Lady kwamba anaamini timu hiyo itatimiza wajibu wake ipoasavyo na kushinda mchezo huo, hivyo kukata tiketi ya kucheza fainali hizo. 
Alisema, kikosi hicho kiliwasili salama nchini humo na kupata sehemu nzuri ya malazi pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi kujiandaa na mchezo huo huku wachezaji wakiahidi ushindi.