SERENGETI BOYS YAMWAGIWA MANOTI
KAMATI ya kuisaidia timu ya kuisaidia timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeimwagia  timu hiyo mil.sita kama motisha kutokana na kuwafunga vija wenzao wa Congo Brazaville jumapili iliyopita
Timu hizo zilikutna kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri huo ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0.
Mmakamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kassim Dewji (pichani)alisema kwamba wameamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kujituma zaidi katika mchezo wao wa marudiano ili waweze kushinda na hatimaye kusonga mbele.
“Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kujituma katika mchezo na vijana wenzao wa Congo Brazaville, hivyo hatuna budi kuwapa fedha hizi kama motisha ya kuwaweezesha kujiandaa vema na mchezo wao wa marudio,”alisema.


MECHI YA SERENGETI BOYS YAINGIZA MIL 23/-
Mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Congo Brazzaville iliyochezwa juzi (Novemba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 23,021,000.

Mapato hayo yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki 15,850 walikata tiketi za sh. 1,000.

Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 5,956,635), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).

Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 250,134, asilimia 45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209, asilimia 20 ya TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 50,027.