RAGE AMREJESHA HANSPOPPE KAMATI YA USAJILI

SIKU chache baada ya kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kutangza kuzivunja kamati zake ndogondogo, mwenmyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage ameanza kuteua wajumbe wa kamati mbalimbali am,bapo ameanza na ya Usajili  ambapo amemrejeshea madaraka yake mwenyekiti wa awali, Zacharia Hanspoppe.
Rage ambayea aliamua kuzivunja kamati hizo kutokana na kutokuwa na mchango wowote katika timu hiyo ambayo iliishia kushika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodaco, amesema kwamba ameamua kumrejesha Hansopppe katika nafasi yake kutokana na kutoa mchango mkubwa katika zoezi la usajili na hasa kutumia fedha zake katika kusajili.
Amesema katika kamati hiyo, Rage atashirikiana na Azim Dewji, Mbunge wa Korogwe Steven Ngonyani maarufu kama 'Prof. Maji Marefu', Muhsin Ruhwey, Sued Nkwabi na wengineo atakaowatangaza baadaye.
Rage ameongeza kuwa hivi karibuni atatatangaza wajumbe wa kamati nyingine baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwateua.
Awali kulikuwa na kamati za Ufundi iliyokuwa chini ya Ibrahim Masoud 'Maestro', Kamati ya Nidhamu iliyokuwa chini Jamal Rwambow, Kamati ya Fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange 'Kaburu' na Kamati ya Mashindabno iliyokuwa chini ya Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi'