PINTO, BENNY KISAKA WAPINGWA DRFA


Juma Pinto na Benny Kisaka 
 MWENYEKITI wa  chama cha waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA) Juma Pinto ni miongoni mwa wadau waliopingwa kuwania uongozi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA). 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Simba amesema kwamba Pinto na Kisaka ambao wameomba kugombea nafasi ya uwakilishi wa Vilabu wamepingwa na Evance Masombo kwa madai ya kutokuwa na elimu ya kidato cha nne.
Amesema wagombea wengine waliopingwa ni pamoja na isack mazilwa  aliyeomba kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambapo amepingwa na Shafii dauda kwa madai ya kuwa si muadilifu. 
Aidha, Mwenyekiti huyo alimtaja mgombea mwingine aliyepingwa ni Muhsin Balhbou ambaye aliomba kugombea nafasi ya uwakilisjhi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) amepingwa na Shafii Dauda kwa kigezo cha kutokuwa na elimu ya kidato cha nne.
 Kamati ya Uchaguzi wa DRFA inatarajiwa kukutana kesho jioni, huku uchaguzi huo ukitarajiwa  kufanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.