NSA JOB KUREJEA ALHAMIS KUTOKA INDIA

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union ya Tanga, Nsa Job (Pichani)anatarajiwa kurejea nchini keshokutwa akitokea nchini India alipokwenda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Nyota huyo alipata maumivu wake wakati akiichezea timu yake dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu bara na baada ya kupata matibabu ya hapa nchini, uongozi wa timu yake ulilazimika kumpeleka India kwa ajili ya matibabnu zaidi.
Ofisa habari wa Coastal Union, Edo Kumwembe ameiambia Sports Lady  kwamba mchezaji huyo ambaye alipatiwa matibabu kwa upasuaji uliokuwa na mafanikio katika hospital ya Saifee iliyopo Mumbai, India.
"Tumewasiliana naye hali yake inaendelea vizuri hivyo keshokutwa (alhamis) atarejea nyumbani na kuja kujiuguza,"alisema Kumwembe