MSIIBEZE KILI STARS, WAPENI SAPOTI VIJANA WETU -TFF


Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewataka Watanzania kutoibeza timu hiyo, badala yake kuiunga mkono. 
Stars ipo nchini humo ikishiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini humo, juzi ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan. 
Rais wa TFF, Leodger Tenga alisema jana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiibeza timu hiyo na hasa kudai wachezaji wake wamezeeka  kitu ambacho si cha kweli kwani wengi wao wana miaka 28 kushuka chini. 
Alisema ni vizuri kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na ari kubwa, hivyo kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo mikubwa. 
Akizungumzia mchezo wa leo, kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen alisema kwamba vijana wake wapo kamili kwa mchezo huo na ili waweze kuifunga Burundi  ni lazima wacheze kwa kasi na pasi za haraka. 
 “Lazima tucheze kwa kasi kubwa sana tena kushinda ule mchezo na Sudan Jumapili kwani Burundi ni timu nzuri lakini tutawabana.”